Jumapili 27 Septemba 2026 - 15:35
“Umma Mmoja” Unajengwa kwa Umoja wa Shia na Sunni; Maadui Wanataka Kuudhoofisha Uislamu kwa Kuwagawa Waislamu

Hawza/ Akhund Mirza Ali, Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Aq-Qala, huku akisisitiza umuhimu wa umoja kati ya Shia na Sunni, amewatuhumu maadui kwa kupanga njama za kuleta migawanyiko miongoni mwa Waislamu, na kusema kuwa; kuheshimiana baina ya madhehebu ya Kiislamu ni sharti la kufanikisha “Umma Mmoja.”

Kwa mujibu wa Idara ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, Akhund Mirza Ali, Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Aq-Qala, aliyasema hayo katika Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa “Kuamshwa Umma wa Muhammad (s.a.w.w.)”, uliofanyika Jumatano, tarehe 1 Mehr 1405, kwa juhudi za Jumuiya ya Kimataifa ya Qademoon. Huku akisisitiza umuhimu wa umoja wa Umma wa Kiislamu, alisema: “Waislamu leo wana wajibu mkubwa zaidi kuliko wakati mwingine wowote wa kuhifadhi umoja na mshikamano wao, na kwa kutegemea umoja, kusimama dhidi ya njama ambazo zinafuatwa kwa lengo la kuupiga Uislamu na kuleta mgawanyiko miongoni mwa Waislamu.”

Akinukuu maneno ya Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) kuhusu kuwa pamoja katika kumuamini Mwenyezi Mungu, Mtume, Qibla na misingi ya pamoja ya Waislamu, alisema: “Pamoja na Waislamu kutofautiana katika baadhi ya masuala, wana mambo mengi ya msingi yanayowaunganisha, na wanapaswa kutegemea mambo hayo ya pamoja.” Akhund Mirza Ali, akirejea aya ya Qur’ani isemayo: «إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ» (Hakika Waumini ni ndugu), alisisitiza kwamba ikiwa Waislamu wanajiona kuwa ni waumini, wanapaswa kuonesha udugu wao wa kidini kwa vitendo na, katika njia ya umoja wa kitaifa na mshikamano wa Kiislamu, kukubali kila mmoja na kutenda kama “mkono mmoja.”

Imamu wa Sala ya Ijumaa wa Aq-Qala pia alirejea aya isemayo: «وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّهِ جَمِیعًا وَلَا تَفَرَّقُوا» (Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja wala msifarikiane), na kusema: “Kushikamana na Kamba ya Mwenyezi Mungu katika uwanja wa kijamii kunamaanisha kuhifadhi umoja, mshikamano wa mioyo, mshikamano wa Waislamu na kuwa na msimamo mmoja.” Aliongeza kwamba; katika mazingira ya sasa, maadui wa Uislamu, wanatumia njia mbalimbali za kuleta mgawanyiko miongoni mwa Waislamu, hususan baina ya Shia na Sunni, na Waislamu wanapaswa kuwa macho ili kuzuia lengo hilo kutimia.

Akhund Mirza Ali, akisisitiza umuhimu wa kuheshimiana baina ya madhehebu ya Kiislamu, alisema: “Umoja hautimizwi kwa kauli mbiu pekee, bali unahitaji kuelewana, kushauriana, kushirikiana, kufanya kazi pamoja kwa moyo wa dhati na kuheshimiana.” Alisema iwapo Waislamu wa Shia na Sunni watakubaliana na kuheshimu matakatifu na shakhsia za kila upande, mazingira ya kuibuka tofauti na mifarakano baina yao yatapungua.

Aidha, akirejea mauaji ya baadhi ya wanazuoni wa Sunni na shakhsia wanaofanya shughuli za kuimarisha umoja na mshikamano wa Kiislamu, alieleza kuwa; vitendo hivyo vinafanyika kwa lengo la kuleta mgawanyiko miongoni mwa Waislamu, na kusema: “Watu wote, wakiwemo wanazuoni na wasiokuwa wanazuoni, wanapaswa kuchukua hatua katika njia ya kuimarisha umoja na kueneza mafundisho ya Uislamu.”

Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Aq-Qala, mwishoni, alisisitiza kwamba Waislamu, kwa kuhifadhi umoja wa kauli, mshikamano wa mioyo na mshikamano wao, wanaweza kusimama dhidi ya njama za kuleta mifarakano na kuchukua hatua za kuimarisha uwepo na nafasi ya Uislamu duniani.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha